Utangulizi
1.1 Mahitaji ya rasilimali watu
Mahitaji ya rasilimali watu kwenye idara ni watumishi 28 ambayo inajumuisha wahandisi wanne, fundi sanifu 8, na fundi bomba 16. Kwa sasa kuna jumla ya watumishi saba (7) ambao mhandisi mmoja (kaimu mkuu wa idara), fundi sanifu (maji) wanne na fundi sanifu wasaidizi (maji) wawili. Hii sawa na asilimia 25 ya mahitaji ya watumishi wote.
1.2 Majukumu ya idara ya maji ndani ya wilaya
Idara ya maji ni mojawapo ya idara 17 katika halmashauri ya wilaya ya mkalama
Kwa kuzingatia mamlaka za serikali za mitaa katika halmashauri ya wilaya ya mkalama, tuna wajibu wa kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa kutoa huduma ya maji kwa jamii ikiwa kama mahitaji muhimu kwa watu.
Zifuatazo ni shughuli ambazo kama idara zinaendelea kuzifanya
a) Kufanya upembuzi yakinifu, kukusanya
b) kufanya utafiti wa maji ardhini ili kuweza kutambua sehemu ambayo itatupa maji ya kutosha ambayo itatumika kama chanzo cha maji
c) Kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwa kuangalia ubora wake
d) Kutunza rekodi za rasilimali za maji
e) Kufanya usimamizi na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maji.
Ili uweze kupata taarifa ya idara kwa undani tafadhali bonyeza hapa
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.