
Maafisa waandamizi kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi nchini (NDC), leo Januari 20, 2026, wamefanya ziara ya kutembelea mradi wa umwagiliaji unaojengwa katika Kijiji cha Ishinsi, Kata ya Msingi, Wilaya ya Mkalama.Ziara hiyo imeongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, Brigedia Jenerali Charles Ndiege, ambaye ameambatana na maafisa mbalimbali kutoka ndani ya nchi pamoja na maafisa kutoka mataifa ya Misri, Malawi, Rwanda, Kenya, Burundi na India.Mradi huo wa umwagiliaji, wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 34, unatarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 10,000 kutoka vijiji vya Ishinsi, Msingi, Kidii pamoja na Ndurumo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.