Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos ameendelea leo ameendelea na ziara yake ya kikazi katika kata za Kikhonda na Kinampundu ya kusikiliza na kutatua kero mbali mbali zinazowakabili wakazi wa kata hizo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa hadhara katika kata za Kikhonda na Kinampundu Bi. Asia Messos amewataka wananchi wa kata hizo kujitokeza kwa wingi kushiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura pamoja na kulinda maadili ya mtanzania.
“Tujitokeze kwa wingi kushiriki uchaguzi, kura yako ni muhimu katika kuleta maendeleo unayoyatamani. Ikifika Novemba 27,2024 kila aliyejiandikisha aende akapige kura. Ukifanya hivyo utakuwa umetendea haki jamii yako inayokuzunguka” DED Asia Messos
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amesema kuwa ili mwananchi uweze kupiga kura huna budi kujiandikisha katika Daftari la Orodha ya Wapiga Kura.
“Lakini ndugu zangu ili uweze kupiga kura, lazima ujiandikishe katika Daftari la Orodha ya Wapiga Kura na zoezi la kujiandikisha litafanyika Octoba 11-20,2024 itakapofika tarehe hii, tujitokeze kwa wingi” DED Asia
Akizungumzia suala la mmomonyoko wa maadili katika jamii, Bi. Asia Messos amewasihi wazazi na walezi wilayani hapa kushirikiana pamoja katika kulinda maadili ya mtanzania kwa kupambana na vitendo viovu kama vile ushoga na usagaji vinavyoshamiri katika jamii zetu,
Aidha Bi. Asia ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha wakazi wa Kikhonda, Kinampundu na wilaya ya Mkalama kwa ujumla kujilinda dhidi ya ugonjwa wa homa ya nyani kwa kuzingatia elimu inayotolewa na wataalamu wa afya wilayani hapa.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.