Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mheshimiwa Moses Machali, leo Januari 27, 2026, amefanya kikao na Watendaji wa Kata na Vijiji, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu Kata pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii, kujadili masuala ya uandikishaji wa wanafunzi wa shule za msingi, kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza pamoja na changamoto ya utoro shuleni.
Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Machali ametoa wito kwa washiriki wote kusimamia kikamilifu mahudhurio ya wanafunzi katika shule zao, akisisitiza kuwa kila mtoto anapaswa kupata haki yake ya msingi ya elimu bila vikwazo.
Aidha, amewataka viongozi hao kushirikiana kwa karibu na wazazi pamoja na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha wanafunzi wote waliodahiliwa wanaripoti shuleni na kuhudhuria masomo ipasavyo.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.