Zao la pamba limetajwa kuwa moja ya mazao yenye thamani kubwa ambalo likilimwa kwa wingi Wilayani Mkalama linauwezo wa kuingizia Halmashauri kiasi Cha shilingi million 177.6 kwa msimu wa 2021/2022.
Hayo yamesemwa na Bw. Juma Salum mkaguzi wa pamba wilaya ya Mkalama na Iramba kutoka bodi ya pamba Tanzania katika mafunzo elekezi juu ya kuongeza uzalishaji na thamani katika zao la pamba.
Aidha Bw. Salum amesema kuwa Serikali kupitia bodi ya Pamba imeweka malengo ya kuzalisha kilo milioni 50 za Pamba katika mkoa wa Singida na kilo milioni 5 katika wilaya ya Mkalama kwa msimu wa 2021/2022.
Baadhi ya wakulima kutoka Kijiji Cha Endasiku Kata ya Mwangeza wameishukuru serikali kushirikiana na Bodi ya pamba Tanzania kutoa elimu ya njia bora za kufuata katika kilimo Cha pamba ambapo wamesema kuwa watatumia tekinolojia waliyoipata na kuacha kilimo Cha mazoea ambapo hapo awali walikuwa wakilima mashamba mkubwa huku mazao yakiwa madogo.
Kata ambazo zinazalisha zao la Pamba ni Mwangeza, Kinyangiri, Msingi, Gumanga, Ibaga, Mpambala pamoja na Kinampundu ambapo tayari elimu imeshatolewa kwa wakulima kwa vijiji 18 kwenye Kata hizo Wilayani Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.