Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia J. Messos, leo 10 Februari 2026 ameongoza kikao kazi na Watendaji wa Kata na Vijiji kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Hospitali ya Wilaya ya Mkalama, akiwahimiza kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato, uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali, msingi na sekondari, pamoja na kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora.

Aidha, amewataka watendaji kuwatangazia wananchi fursa za mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa katika karakana ya Shule ya Msingi Nduguti, ikiwemo ufundi seremala, ushonaji na batiki, ufundi wa magari, TEHAMA, pamoja na ufundi wa kuchomeleaji, kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira hususan kwa vijana
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.