Katika kuadhimisha Kilele cha Kichaa cha Mbwa Duniani (World Robbies Day) Wizara ya Mifugo na uvuvi kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali Education for African Animals Walfare(EAAW) imetoa chanjo ya Mbwa wapatao 432 wilayani Mkalama.
Chanjo hiyo imetolewa katika Vijiji vya Yulansoni , Msingi pamoja na Maziliga wilayani Mkalama Mkoa wa Singida.
Akiongea katika zoezi hilo Afisa Mifugo wilaya ya Mkalama Elias Mbwambo amesema kuwa zoezi hili ni kutekeleza takwa la Kisheria chini ya sheria Na. 17 ya mwaka 2003 ya udhibiti wa magonjwa ya wanyama na sheria Na.19 ya 2008 ya haki na ustawi wa Wanyama rafiki.
Aidha Mbwambo aliongeza kwa kuwataka wananchi kuzingatia zoezi hili adhimu pindi linapokuja kwao kwani chanjo inatolewa bure na itawakinga wanyama na ugonjwa wa kichaa cha Mbwa unaopelekea kupoteza wanyama na kutumia gharama nyingi pindi Mbwa wanapong’ata watu kutokana na matibabu kuwa ghali.
Mkurugenzi wa shirika la Education for African Animals Walfare Ayubu Nnko amesema toka mwaka 2019 wamekuwa wakishirikiana na Wilaya ya Mkalama katika kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha Mbwa ambao awali ulikuwatishio kubwa ukilinganisha na sasa .
Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wadau wa maendeleo wilayani Mkalama kushirikiana na Idara ya mifugo na uvuvi kujitokeza kuwekeza kwenye Wanyama kwani nao wanahaki ya kuishi na kuhudumiwa kama vile kupatiwa chanjo na mahali salama pa kuishi.
Baadhi ya wafugaji wameishukuru serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoa dozi 500 za chanjo ya Mbwa na kuongeza kuwa chanjo hiyo itawasidia wanyama wao kuwa salama kwani wanawasaidia katika ulinzi pindi wanyama waharibifu na wezi wanapoenda kuiba.
’’Mbwa ni wanyama rafiki maana wanatusaidia kwenye ulinzi tunaishukuru serikali kuona umuhimu wa wanyama wetu na kutuletea chanjo ya kutibu kichaa cha Mbwa , nashauri watu wengine ambao hawajawaleta Mbwa walete wapatiwe chanjo’’ alisema Isron Japhet
Kilele cha Kichaa cha Mbwa huadhimishwa kiala ifikapo Septemba 28 kila mwaka.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.