Mkalama, Septemba 3, 2025 – Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali, ameongoza kikao cha tathmini ya lishe kwa robo ya nne kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Kikao hicho kiliwahusisha waganga wafawidhi, wakuu wa idara na vitengo, maafisa lishe wa wilaya pamoja na watendaji wa kata kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mkalama.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Machali amewataka wajumbe kuongeza juhudi katika kuboresha lishe ya wananchi kwa kuhimiza matumizi ya unga ulioongezewa virutubisho vya madini, pamoja na kuzingatia ulaji wa makundi matano ya chakula kwa kila mlo ili kuimarisha afya ya mwili na akili.
Aidha, amewataka wajumbe hao kuwa mabalozi wa lishe kwa jamii zao kwa kutoa elimu endelevu kuhusu umuhimu wa lishe bora, huku akisisitiza kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yameendelea kuwa changamoto kubwa kwa jamii.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.