Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovick, amefanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Mkalama kukagua zoezi la utoaji wa huduma za kibingwa zinazotolewa na madaktari bingwa wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wilayani hapa.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Dkt. Ludovick amewapongeza madaktari bingwa hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka wananchi wa Wilaya ya Mkalama pamoja na wilaya jirani kujitokeza kwa wingi kuchangamkia huduma hizo za kibingwa.
Aidha, Dkt. Ludovick ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa jitihada zake za kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa karibu na maeneo yao, hatua inayosaidia kupunguza gharama na muda wa kufuata huduma hizo katika hospitali za mbali.
Katika ziara hiyo, Dkt. Victorina Ludovick aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, wataalamu mbalimbali kutoka ofisi ya Mkoa wa Singida pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkalama.
Zoezi hilo la madaktari bingwa linaendelea kuanzia tarehe 6 hadi 10 Oktoba, 2025, likihusisha utoaji wa huduma za matibabu pamoja na mafunzo kwa watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.