Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe .Sophia Kizigo amewataka watendaji wa kata na wahudumu wa afya kuongeza kasi ya uhamasishaji kwa jamii ili wajitokeze kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO 19 ya awamu ya pili ijulikanayo kwa jina la SINOPHARM baada ya kufanikiwa kumaliza ya awamu ya kwanza iliyojulikana kwa jina la JANSON JANSON.
Amesama hayo mapema leo wakati akifungua kikao cha Uhabarisho wa chanjo ya UVIKO 19 kilichojumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo watendaji wa Kata na wahudumu wa Afya kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha Mhe.Kizigo amewataka watendaji ngazi ya Kata,Wahudumu wa Afya ,wakuu wa Idara na Vitengo kwa umoja wao kuhakikisha wanatoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya UVIKO 19 kwani ni salama na imethibitishwa na Wizara ya Afya.
‘’Tulifanya kikao mara ya kwanza na Viongozi wa wilaya kuhusu uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO 19 ambapo mwanzo tulikuwa na JANSON JANSON, kama wilaya tulifanya vizuri kwa kumaliza chanjo tulizopewa ,baada ya kikao hicho tuliona ipo haja ya kukaa na watendaji wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya kata ili kuongeza nguvu ya uhamasishaji.’’ Alisema Mhe.Kizigo Dc Mkalama.
‘’Sasa tumeletewa chanjo aina ya SINOPHARM dozi 4200 hizi zitatolewa mara mbili tofauti na JANSON JANSON iliyokuwa inatolewa mara moja , tukatoe elimu kwa Wananchi kuwa ni Muhimu mtu akipata chanjo atatakiwa kukaa siku 28 ndipo arudi kuchoma nyingine,hivyo ninategemea baada ya kikao hiki kila mtu kwa nafasi yake atakuwa mwalimu mzuri kutoa elimu juu ya ubora na umuhimu wa chanjo hii ni matumaini yangu hamtaniangusha.’’Aliongeza Mhe.Kizigo .
Naye mratibu wa chanjo wilaya ya Mkalama Duncan Kifaruka amesisitiza ushirikiano baina ya jamii na wataalamu ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa kuongeza uwezo wa kutoa huduma kwa sehemu ngumu kufikika ,umuhimu wa ufuatiliaji wa dozi ya pili huku elimu na ushawishi ukiendelea kutolewa kwa jamii ili chanjo ya UVIKO 19 ikubalike tofauti na kipindi cha mwanzo ambapo chanjo hiyo ilichukuliwa kwa Mtazamo hasi.
Afisa Lishe wilaya ya Mkalama Bi.Eliwandisha Kinyau amesisitiza lishe bora na ulaji unaoshauriwa katika kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo ameshauri ulaji unaozingatia makundi matano ya chakula kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mwili katika kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili kwani magonjwa ya kuambukiza ikiwemo UVIKO 19 hubadili ufanyanji kazi wa mifumo mbalimbali ya mwili ikiwemo mfumo wa chakula.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.