Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ametoa wito kwa wanawake wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii kwa ajili ya kupata nafasi ya kupigania haki za wanawake wanaoathirika na mfumo dume.
Kauli hiyo ameitoa Machi 5, 2025 wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake kiwilaya yaliyofanyika katika kijiji cha Nkalakala, kata ya Nkalakala wilayani hapa.
“Ili muweze kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili katika jamii, jitokezeni kugombea nafasi uongozi kwa kufanya hivi mtaweza kupigania haki za wanawake wanaofanyiwa ukatili katika jamii zetu”
Mhe. Machali amewasihi wanawake kuachana kuchukiana wao kwa wao bali wapendane na kuheshimiana “Ukiona mwanamke yeyote amekuwa kiongozi mpe maua yake, msichukiane, lazima tuishi kwa kupendana” Mhe Machali
Akizungumzia suala la kuwalinda watoto wakike dhidi ya ukatili wa kijinsia, Mhe. Machali amewataka kina mama kuhakikisha wanawasomesha watoto wakike, pamoja na kuwafundisha watoto na kuwafundisha watoto wakiume kuwa na nidhamu kwa dada zo.
Aidha Mhe. Machali amewakumbusha wanawake na wanaume kwa pamoja walio kwenye ndoa kuachana na michepuko ili kuepuka madhara kama vile kuleta magonjwa kwenye ndoa pamoja na kusababisha uvunjifu wa maadili katika jamii.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Wanawake Duniani katika wilaya ya Mkalama yalienda sambamba na utoaji zawadi kwa wanafunzi wakike walioshindanishwa katika shindano la uandishi wa Insha kwa wanafunzi wa shule za msingi wilayani hapa pamoja na uchangia damu, na zoezi la upimaji UKIMWI.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.