Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amezitaka jamii za wafugaji na wawindaji( Wahdazabe) kuacha kujichukulia sheria mkononi katika kugombea mipaka ya Ardhi wakati mgogoro wao unashughulikiwa na mamlaka husika.
Amesema hayo Januari 18, 2024 wakati akiongea na jamii hizo katika kijiji cha Munguli kitongoji cha Kipamba kata ya Mwangeza Wilaya ya Mkalama.
Bi. Messos amewaeleza namna serikali ilivyojipanga kushughulikia migogoro mbalimbali na kuwataka kuwa watulivu wakati mgogoro huo unapatiwa ufumbuzi.
‘’ kweli hata sisi tumesikitishwa kuona jamii hizi zimekuwa na mgogoro na kufikia hatua ya kuharibu mizinga ambayo serikali ilitioa kwaajili ya jamii hii ya wahadzabe kujiongezea kipato, lakini ikatokea jamii nyingine inaharibu mizinga hiy. Nawahakikishia mgogoro huu utapatiwa ufumbuzi maana tayari umeshafika ngazi ya Mkoa’’ Aliongeza DED Messos.
Pamoja na hayo amewataka wananchi kutii mamlaka kwa kufuata sheria zilizopo ili kupata haki zao sambamba na kuacha tabia ya kulea wahalifu wanaosababisha migogoro katika jamii, na mamlaka zilizopo kuchukua hatua za kisheria kwa wanaokwenda kinyume na utaratibu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.