Baadhi ya wakulima na washiriki wa mafunzo ya kilimo cha zao la Pamba katika Vijiji vya Kinyangiri,Lyelembo na Yulansoni wameishukuru serikali kupitia bodi ya Pamba pamoja na kampuni ya Biosustain kuendelea kutoa elimu juu ya Kilimo Bora cha Pamba katika kuongeza thamani na uzalishaji wa zao hilo.
Wameyasema hayo katika mafunzo elekezi ya Kilimo cha zao la Pamba yanayoendelea wilayani hapa kwa Vijiji vinavyolima zao hilo.
Aidha wamesema ujuzi wanaoupata watautumia vyema katika kuongeza thamani ya uzalishaji wa Pamba katika maeneo yao kwa kufuata kanuni Bora 10 za Kilimo huku wakiwaomba wataalamu kuwatembelea mara kwa mara na kutoa ushauri kwa wakulima.
Kwa upande wake Afisa mazao wilaya ya Mkalama Bw.Daniel Jacobo amewataka wakulima kulima mazao ya chakula na biashara ili kuwa na akiba ya chakula pamoja na mazao ya biashara yatakayowasaidia kuongeza uchumi wa familia pamoja na wilaya kwa ujumla.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.