Watendaji wa kata pamoja na wajumbe wote wa sensa ya watu na Makazi wilayani Mkalama wametakiwa kuihamasisha jamii pamoja na vijana wenye sifa za kutuma maombi ya ajira za muda kwaajili ya zoezi la Sensa ya watu na Makazi linatarajiwa kufanyika tar 23 mwezi Agosti Mwaka huu.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Kizigo amesema hayo katika kikao kazi cha kwanza cha wajumbe wa kamati ya sensa ya watu na Makazi wilayani Mkalama kilichofanyika Katika ukumbi wa Sheketela uliopo halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
Aidha Mhe. Kizigo ameongeza kuwa Kila mtu akisimama kwa nafasi yake kuhamasisha zoezi la Sensa itapelekea Serikali kupata idadi kamili ya Wananchi na kusaidia kupanga bajeti sahihi ya Nchi katika suala la Elimu, afya, Maji pamoja na mambo mengine.
Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya, Mratibu wa Sensa Wilaya ya Mkalama Bw.Daniel Tesha alieleza shughuli zinazoendelea Kwa Sasa kuwa ni kuendelea kutoa elimu ya hamasa Kwa wananchi Ili washiriki zoezi la Sensa Kwa kamati za sensa pamoja na kuratibu zoezi la kuwapata makarani na wasimamizi wa sensa Kwa Mwaka 2022..
Tanzania imekua ikifanya sensa Kila baada ya miaka 10 na Kwa Mwaka huu inatarajia kufanya Sensa Agosti 23 ambapo itakua ni sensa ya sita (6) tangu uhuru na zoezi hili linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya Takwimu sura ya 351.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA".
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.