Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Messos, amewataka wafanyabiashara, wajasiriamali pamoja na watumishi Wilayani Mkalama kutumia ipasavyo huduma za kifedha ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na taasisi kwa ujumla.
Bi. Messos alitoa wito huo mapema leo Agosti 19, 2025, katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, wakati akifungua Kongamano la Huduma Ndogo za Kifedha.
Ameeleza kuwa wafanyabiashara wengi wamezoea kutumia taasisi za kifedha kama benki pekee, lakini akasisitiza pia umuhimu wa kutumia Mfuko wa UTT AMIS, taasisi ya serikali iliyo chini ya Wizara ya Fedha, inayosaidia wananchi kujiwekea akiba na kuwekeza katika masoko ya mitaji.
Aidha, Bi. Messos alisisitiza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imeendelea kutoa mikopo bila riba kwa makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuinua kipato na kukuza uchumi wa wananchi.
Amewataka wanavikundi vinavyopatiwa mikopo hiyo kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa ili ziwe chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwao na jamii inayowazunguka.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.