Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Kizigo amewashukuru wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) kuibua hoja zenye ustawi kwa wilaya ya Mkalama ambapo amewahakikishia kufanyia kazi maazimio yote yaliyotokea kwenye kikao hicho.
Amesema hayo mapema leo wakati akifunga kikao cha Kamati ya Halmashauri ya wilaya ya Mkalama kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya wilaya ya Mkalama
Aidha Mhe.Kizigo amesema kuwa kikao hicho kimejadili mambo muhimu na yenye ustawi kwa wilaya ya mkalama ikiwa ni pamoja na hali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo , uchumi, kilimo ,elimu pamoja na afya ambapo aliwataka kamati hiyo kuhakisha wanawashirikisha wananchi pia katika kuunga mkono juhudi za serikali.
Katika hatua nyingine baadhi ya wajumbe wameshauri mambo mbali mbali hususani katika kukuza kiwango cha taaluma wilaya ya Mkalama ambapo walishauri serikali kuajiri watumishi katika sekta ya elimu ,kudhibiti utoro shuleni pamoja na wajumbe wa kamati na bodi za shule kushiriki kwenye vikao ili kujionea changamoto na kuweza kuzitatua.
Pamoja na mambo mengine wamekumbushwa kuwashauri wananchi kutunza chakula kwani kunauwezekano mkubwa wa bei kuendelea kupanda kutokana na kuchelewa kwa mvua huku jamii ikiendelea kuhamasishwa kulima zao la alizeti ili kufikia lengo la serikali la kujitosheleza kwa mafuta ya kula.
Kikao hicho kimehusisha wakuu wa idara na vitengo,watendaji wa kata,kamati ya usalama wilaya ya Mkalama,Waheshimiwa madiwani pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.