Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Sophia Kizigo amewapongeza wahitimu wa mafunzo ya jeshi la Akiba kwa kuhitimu mafunzo yao yaliyoanza August 9 mwaka huu huku akiwataka kuwa mfano wakuingwa na jamii kwakuonyesha uzalendo na uwajibikaji kwa kufanya kazi za uzalishaji mali ili kuongeza pato lao,jamii na wilaya kwaujumla.
Ameyasema hayo leo November 11, 2021 wakati wa hafla fupi yakufunga mafunzo ya jeshi la akiba yaliyofanyika Kijiji cha Kinyangiri Kata ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Aidha Mhe.Kizigo amewataka wahitimu kuwa chachu kwa wengine kwakuonyesha uzalendo wa kweli kwa maslahi mapana ya Nchi pia wakatumie elimu waliyopata kwa kupambana na madawa ya kulevya na rushwa.
Katika hatua nyingine amewataka kujiunga na vikundi ili wapate mikopo itakayowasaidia kufanya kazi za uzalishaji mali ambapo amesema kuwa serikali itawapa kipau mbele kwenye shughuli za serikali pindi zinapotokea .
“niwapongeze sana vijana kwanza kwa kuvumilia na leo mmehitimu mafunzo yenu ya jeshi la akiba, natumai sasa mmeshakua ndugu hivyo umoja wenu ukaimarike kwa kujiunga na vikundi ili serikali iwape mikopo kwaajili ya shughuli za uzalishaji na serikali itawapa kipaumbele kwenye shughuli mbalimbali kwani tayari nyie mnajua nini maana ya uzalendo katumieni mafunzo yenu vizuri kwakuisaidia jamii kwenye ulinzi na usalama katika kupambana na uhalifu’’.Ameongeza Dc Kizigo.
Afisa Mteule Daraja la pili Tobias Kahemele amewapongeza Vijana waliomaliza mafunzo salama ambapo kwa ujumla wao ni 51 wakiume wakiwa 41 na wakike 4 huku akitaja baadhi ya changamoto kwa wanafunzi walioshindwa kumaliza mafunzo kuwa ni utoro pamoja na wazazi kutojua umuhimu wa mafunzo hayo kwakuwashawishi vijana wao wasijiunge na mafunzo ambapo ameiomba serikali kutunga sheria ya kuwawajibisha wanaoacha mafunzo .
Akisoma Risala kwa Mgeni rasmi miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo Shabani Mohamed amesema kwa muda wa miezi minne wamejifunza uzalendo kwa Nchi,nidhamu,utiifu pamoja na kushiriki kazi za kijamii katika shule ya Msingi Kinyangiri , kupata elimu ya mapambano ya dawa za kulevya ,rushwa pamoja na usalama wa raia huku wakiiomba serikali kuwapa nafasi za kwanza katika shughuli mbali ikiwa ni pamoja na ulinzi kwenye makampuni, kusimamia mitihani pamoja na kujiiunga na jeshi la kujenga Taifa(JKT) pindi nafasi zinapopatikana.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.