Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Binilith Mahenge amewataka viongozi kuwasikliza Wananchi na kutatua kero zao kwani wapo kwaajili ya kutumika na sio kutumikiwa.
Amesema hayo leo wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani Mkalama katika Kata ya Iguguno kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida
‘’viongozi nikuhakikisha mnapokea kero za wananchi ,viongozi ni lazima muwe wanyenyekevu kwa wananchi wenu sio mwananchi anakuja kama Yule mzee pale mnakua hamwasikilizi inakua sio jambo jema’’ alisema RC MAHENGE.
Rc Mahenge amesema kuwa pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika ziara yake pia alitaka kuwafahamisha wananchi wa wilaya ya Mkalama namna serikali inavyotoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Sekta ya Elimu, Afya , Maji, Umeme pamoja na barabara na kusema ni jambo la kujivunia kwa mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya Sita kufanya mambo makubwa ndani ya wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Hata hivyo Rc Mahenge aliwatoa wasiwasi wananchi wa Kijiji cha Iguguno kuwa kero zote walizowasilisha zitafanyiwa kazi kwani katika ziara yake amekua akitembea na wakuu wa Taasisi na wataalamu wa Idara zote za serikali ambao wamekua wakijibu nakueleza namna serikali inavyofanya kazi zake na inavyoendelea kufanya katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine alitumia fursa hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika ukusanyaji wa mapato ambapo Hadi kufikia Leo June 29 Halmashauri imefanikiwa kuvuka lengo na kukusanya mapato Kwa asilimia 101 Sasa ambapo alisema hii inatokana na uimara na ushirikiano liopo kati ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya pamoja na wataalamu mbalimbali wilayani Mkalama .
Awali akimkaribisha Rc , Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema kuwa wilaya yaMkalama imebarikiwa kuwa na Ardhi nzuri inayostawisha mazao ya kila namna ikiwepo zao la Korosho ambalo lililimwa katika Kijiji cha Gumanga kata ya Gumanga na sasa kama wilaya wamepata mavuno mazuri ya zao hilo hivyo kuahidi kufanyika kwa kampeni kwa wilaya nzima ili zao hilo lilimwe kote wilaya hapa.
Pamoja na hayo Dc Kizigo aliwataka wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za serikali , pamoja na kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi Agost 23 mwaka huu na kuwaahidi wananchi wa Kata Iguguno kujiandaa kukesha na mwenge wa huru siku hiyo kwani wilaya imetambua mchango wa wananchi hao kwenye shughuli mbalimbali za wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Asia Messos alisema kuwa Wilaya ya Mkalama imepokea kiasi cha Shilingi Billion Tano million mia nne na nne laki Nne na themanini na nne elfu mia nne sabini na tisa katika sekta za Afya , Elimu , Maji pamoja na kujenga nyumba ya Mganga katika hospitali ya wilaya nakusema kukamilika kwa nyumba hiyo itaweza kutumiwa na familia Tatu na kupunzuza uhaba wa nyumba za watumishi kada ya afya , huku shilingi Mil 150 ikiwa ni kwaajili ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.