Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali inazidi kuzaa matunda kwa kusikiliza na kutatua kero mbalimbali Wilayani hapa zikiwemo migogoro ya Ardhi, Barabara, Maji, Elimu pamoja na Afya.
Akiongea na wananchi wa vijiji vya Kinankamba,Ikungu Kata ya Gumanga Mhe. Machali amewaeleza wananchi lengo la serikali kuwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora katika Nyanja mbalimbali huku akitoa fursa kwa wananchi hao kutoa kero mbalimbali ambapo amejibu kero zote huku zingine akizotolea maelekezo ya kuanza kushughulikiwa mapema iwezakanavyo.
Aidha akitoa majibu kuhusu changamoto ya umeme ambayo imeonekana kuwa ni tatizo kwa baadhi ya vitongoji , Mhe. Machali ameieleza jamii lengo la serikali kuwa nikufikisha umeme katika maeneo yato na ilianza na vijiji ambapo kwa Wilaya ya Mkalama Vijiji vyote 70 vimeshapata umeme na kuongeza kuwa mpango wa serikali sasa ni kuhakikisha vitongoji vyote vinapata umeme.
Mhe. Machali ametatua migogoro mbalimbali baina ya mwananchi na mwananchi katika Kijiji cha Ikungu ambayo ilidumu kwa muda mrefu huku wakimuahidi kuwa wataendeleza ushirikiano kama waliyokuwa nayo nyuma kwaajili ya maendeleo ya Kijiji chao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gumanga Mhe. John Mkwega amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa juhudi zake za kuhudumia wananchi katika kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.