Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amewataka watahiniwa wa kidato cha Sita kujiandaa kikamilifu kuingia kwenye soko la ajira lenye ushindani Mkubwa kutokana na kukua Kwa Sayansi na Teknolojia Duniani.
Ameyasema hayo wakati wa hotuba yake kwenye mahafali ya tano ya kidato Cha Sita ya Shule ya Sekondari Iguguno iliyopo wilayani Mkalama Mkoani Singida ambapo alisema kuwa ni muhimu wanafunzi kujifunza mambo mengi kama elimu ya uongozi kwani itawasaidia kufanya kazi popote, kuwa na uwezo wa kuwasiliana kwakutumia lugha za picha kuwa na uwezo wa kusikiliza kitu kitakachopelekea kutoa huduma zilizo bora kwa jamii.
Mhe. Kizigo Aliongeza kuwa ulimwengu wa Sasa ni waushindani Mkubwa tofauti na awali hivyo kuwataka kutumia elimu waliyoipata kujua mambo mengi ya kidigitali ( Digital Market) Ili kuweza kupokea fursa zinazokuja kutokana na fani walizosomea pia kufanya mambo mengine ikiwemo kufanya biashara mtandaoni pamoja nakutafuta wateja wapya mtandaoni.
Pamoja na hayo alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi, wazazi pamoja na Walimu kwakushirikiana kuongeza ufaulu shuleni hapo ambapo Aliongeza kuwa Ili ufaulu uongezeke ni muhimu mafiga hayo matatu yashirikiane huku akiwataka wanafunzi hao kutumia vizuri muda uliobaki kujiandaa na mitihani ya kuhitimu kidato cha sita inayotarajiwa kuanza mapema mwezi Mei.
Awali akisoma risala Kwa Mgeni rasmi Mwl Stephano Mafole alisema kuwa Mwaka 2022 wanatajia kuongeza ufaulu Kwa Madarasa ya mitahani ambapo alisema kuwa wanatarajia kufaulisha wanafunzi Kwa daraja la kwanza na la pili tu na kuongeza ufaulu kutoka asilimia 93 Kwa kidato Cha pili , asilimia 94 Kwa kidato Cha Nne na asilimi 100 Kwa kidato Cha Sita ya Mwaka 2021.
Pamoja na hayo aliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kuwapatia miradi ya maendeleo kwa kujenga vyumba sita vya Madarasa kwani imesaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia hivyo kupelekea wanafunzi kusoma mahali pa zuri na kuongeza kiwango Cha taaluma shuleni hapo.
Shule ya Sekondari Iguguno ilianzishwa Mwaka 2000 ikiwa ni shule ya kidato Cha kwanza hadi cha Nne, na mnamo Mwaka 2016 shule hiyo iliongezewa hadhi ya kuwa na kidato Cha tano na sita kwa michepuo ya Sanaa Kwa tahasusi za HGK, HGL na HGE na Kwa Sasa ina jumla ya wanafunzi 1,124 kati ya hao wavulana ni 502 na wasichana wakiwa 623 ,kati ya hao ni wanafunzi 109 wanatarajia kufanya mtihani wa kidato Cha Sita Kwa Mwaka 2022 ikiwa wavulana ni 70 na wasichana 39.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.