Jamii ya wawindaji na wafugaji ya Wahadzabe iliyopo katika kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza wilayani Mkalama imepokea vifaa kwaajili ya ufugaji wa nyuki vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milion miamoja Arobaini na Tatu(Tsh mill. 143.3)ili kuwasaidia katika ufugaji wa kisasa na kuacha ufugaji wa kienyeji kama walivyozoea.
Akikabidhi vifaa hivyo katika Kitongi cha Kipamba Kijiji cha Munguli Mkuu wa wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alisema kuwa vifaa hivyo vikawe chachu ya kuboresha ufugaji wao na kujiongezea kipato pia kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwani ni chakula na ni dawa pia.
‘’kwa namna ya kipekee niwashukuru wadhamini kutoka Mfuko wa Kimataifa wa mazingira kwa Kinyiramba wanaitwa (Global Environmental Facility) kudhamini mradi huu na kutoa zaidi ya Millioni mia kwenye mradi na kuhakikisha tunapata maendeleo endelevu huku tukitunza mazingira ,ni jambo kubwa, pia niwashukru Ofisi ya Makamu wa Rais wizara ya Muungano na Mazingira kuona ipo haja na sisi wanamkalama kupata mradi mkubwa kama huu pamoja na kuwa tuna sifa za kuwa na msitu lakini Tanzania ina Misitu mingi jamani ni jambo la kipekee sana’’ Aliongeza Dc Kizigo.
Aidha Dc Kizigo alitumia fursa hiyo kuitaka jamii hiyo kutunza vifaa walivyopokea leo ili viwanufaishe kwani serikali imewekeza fedha nyingi kuhakikisha wanapata faida na kuongeza uzalishaji ili inapofika mwisho wa mradi huu wawe wameweza kujitegemea na kukuza mtaji kwa masilahi mapana ya jamii hiyona wilaya kwa ujumla .
Afisa Mazingira wilaya ya Mkalama Amon sanga amesema kuwa jumla ya Mizinga 1100 imekabidhiwa pamoja na vifaa vya urinaji asali vitakavyosaidia jamii ya Wahadzabe kufuga nyuki na kurina asali kisasa ili kuongeza thamani ya uzalishaji wa zao la Asali ambalo linategemewa na jamii hiyo kama chakula pamoja na dawa .
‘’Wilaya ya Mkalama ni miongoni mwa wilaya Tano zinazotekeleza mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula katika maeneo kame Tanzania ambazo ni Nzega ( Tabora) Magu ( Mwanza) Kondoa (Dodoma) pamoja Micheweni (Kaskazini Pemba –Zanzibar) na katika wilaya zote hizo tano wilaya ya Mkalama ndio imepata bahati na hii inatokana na ukweli tu kwamba wilaya ya Mkalama imekidhi vigezo vya kuwa na Msitu wakutosha na wenyenye ushawishi mkubwa, wilaya ya Mkalama ina msitu wa Hekari elfu moja mia sita hamsini na sita katika kitongoji cha Kipamba kijiji cha Munguli.’’ Alisema Sanga.
Aliongeza kuwa huo ulikuwa ni ushawishi tosha kwa wafadhili wa mradi kuona kuwa walengwa watanufaika ma mradi huo moja kwamoja ukizingatia katika kijiji cha Munguli kuna jamii ya Kabila la Wahadzabe ambao wanategemea zao la asali kama chakula.
Kabla ya zoezi la kukabidhi vifaa hivyo Afisa nyuki wilaya ya Mkalama Abdul Alli alieza matumizi ya vifaa hivyo kuanza hatua ya kuingia nyuki hadi kuvuna zao la asali pamoja na namna ya kuchakata ili kupata asali yenye ubora bila kuathiri kizazi ya chuki kilichopo huku akitaja faida za kufuga nyuki kitaalamu itaongeza uzalishaji wa zao hilo kuvuna zaidi ya mara tatu kwa mwaka ambayo itaongeza thamani ya zao hilo na kukuza kipato kwa Vikundi vya uzalisha , familia pamoja na jamii kwa ujumla.
Mwenyekiti wa jamii ya Wahadzabe Edward Mashimba ameishukuru serikali kupitia mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula kwa kuwajali na kuona jamii hiyo inafaa kuwa na mradi endelevu na kusema ni upendeleo wa kipekee kwa serikali kuwekeza zaidi ya Million mia moja kuhakikisha wanaingia katika dira ya dunia ambapo ameahidi kulinda vifaa hivyo ili viwasaidie katika kuongeza tija kwenye zao la asali na kuacha kufuga nyuki na kuvuna kienyeji jambo lililopelekea kuua zao la nyuki kwasababu walikuwa wanachoma moto nyuki ndipo wapate asali.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.