Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe Moses Machali amewataka wafanyabiashara wilayani Mkalama mkoani Singida kuuza sukari kulingana na bei elekezi ya serikali na kuwataka wasifiche sukari kwani atayebainika kufanya hivyo atachekuliwa hatua kali za kisheria
Kauli hiyo ameitoa Januari 24,2024 mara baada ya kumaliza zoezi maalum la kukagua na kuwabaini wafanyabiashara wanaouza sukari bei juu tofauti na maelekezo yaliyotolewa na serikali kupitia bodi ya taifa ya sukari nchini.
"Bei ya rejareja ya sukari katika mkoa wa Singida kwa mujibu wa Bodi ya Sukari nchini haipaswi kuzidi shilingi 3000.Tutakayemkuta anauza sukari zaidi ya shilingi 3000 tutamkamata. Mnasababisha maisha ya wananchi yanakuwa magumu. Hatuwezi kuruhusu hilo" Mhe. Moses Machali
"Wafanyabiashara wa Mkalama msiuze sukari kwa bei rejareja zaidi ya shilingi 3000, na wananchi wa Mkalama mkisikia popote mfanyabiasnara anauza sukari kwa bei ya rejareja zaidi ya shilingi 3000 toa taarifa tumshughulikie. Pia wafanyabiashara wa Mkalama msifiche sukari, ukabainika tutakukamata kwa kosa la uhujumu uchumi. Tutakushughulilia" Mhe. Moses Machali
Aidha Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewakumbusha wafanyabiashara hao kuhakikisha wanakuwa na stakabadhi za malipo pindi wanaponunua sukari kutoka kwa wasambazaji wakubwa ili kuweza kubaini kwanini wanauza bei kubwa tofauti na maelekezo ya yaliyotolewa na serikali kupitia Bodi ya sukari nchini.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.