Habari Njema na kubwa kwako Mwananchi wa Wilaya ya Mkalama na Tanzania kwa ujumla ni kwamba Wilaya ya Mkalama imeanza mchakato wa Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu utakapokuwa na uwezo wa kubeba watazamaji 45,000.
Uwanja huo bora kabisa na wa kisasa unaotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.6 unajengwa katika kijiji cha Maziliga na tayari eneo hilo limeshasafishwa huku hatua ya kulisawazisha au kufanya ‘’levelling’’ kama inayojulikana kitaalam ikitarajiwa kufanyika Wiki ijayo.
Mbali na Mpira wa Miguu, uwanja huo utakuwa na viwanja vya ndani vya michezo ya Mpira wa Kikapu, Mpira wa ikono, Mpira wa Pete, Mpira wa Wavu na sehemu ya Mashindano ya riadha.
Ujenzi huo unaoratibiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Mkalama chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Mhandisi Lameck Itungi unatarajiwa kukamilika Julai 2019 ambapo zaidi ya matofali 5000 kati ya 27,000 yanayohitajika kwa ajili ya ujenzi wa Ukuta wa Uwanja huo yameshafyatuliwa.
Kwa Mujibu wa Mhe. Itungi jumla ya mali zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 800 zimeahidiwa kutolewa na wadau mbalimbali ambapo kiasi kingine cha Fedha kinatarajiwa kukusanywa katika Harambee itakayofanyika septemba 9 mwaka huu.
“Mgeni rasmi katika harambee hiyo anatarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi wote wa Wilaya ya Mkalama na Watanzania kwa ujumla mjitokeze kuunga Mkono jitihada hizi za dhati kwa ajili ya kuendeleza sekta ya Michezo Mkalama na Tanzania kwa ujumla” Alisihi Mhe. Itungi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.