Imebainika kuwa Mkataba wa lishe umesaidia kupunguza udumavu Wilayani Mkalama kutoka 42% kwa takwimu za mwaka 2010 hadi 34% kwa takwimu za 2015 na kutoka 34% hadi 32% kwa mwaka 2020 huku takwimu za Mkoa zikionyesha udumavu kupungua na kufikia 29%.
Hayo yamesemwa na Bw.Abdala Njelu akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mkalama katika kikao cha usimamizi wa Mkataba wa Afya na Lishe katika ngazi ya Kata , Vijiji na Mtaa iliyofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha Bw. Njelu amesema kuwa kama Wilaya imekusudia kupunguza udumavu mpaka kufikia 0% ambapo pia amewataka watendaji wa Kata, wataalamu wa afya kwakushirikiana na jamii ili kuhamasisha masuala ya lishe na vyakula vinavyoshauriwa vinayotokana na makundi yote matano ya vyakula.
Pamoja na hayo amesema kuwa malengo ya mikataba hii ni sawa na ile aliyosaini waziri wa Nchi OR TAMISEMI na Wakuu wa Mikoa yote Tanzania bara mnamo tar 19 Disemba 2017 na mikataba hiyo iliyoanza kutumika tar 1 January 2018 ikiwa ni kufanikisha suala la kuboresha lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika ngazi za Kata na Vijiji.
Kwa upande wake Afisa lishe Wilaya ya Mkalama Bi Eliwandisha Kinyau amesema kuwa Wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kupitia siku ya Afya na lishe na Mikutano ya hadhara kwakuelekeza namna sahihi ya kuuandaa chakula na lishe kwa watoto kwakuzingatia Makundi matano ya vyakula.
Pia ametaja vyakula vinavyoongeza damu kwa wingi kuwa lazima vitokane na makundi matano ya vyakula kuwa ni mboga mboga za kijani pamoja na matunda ,Madini ya chuma pia nyama ikishauriwa kuliwa kwa kiasi huku akisisitiza watu wafanye mazoezi ili kuweka miili yao vizuri kwa kuimarisha Afya ya mwili na akili.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.