Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka watendaji kata, Watumishi wa Afya, Wakuu wa Idara zinazohusika na suala la lishe kutimiza wajibu wa kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe ili kuwa na jamii yenye afya bora.
Wito huo ameutoa Mei 26,2024 wakati wa Kikao cha Tathimi ya Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Mkalama.
“Twendeni tukafanye kazi tuondoe alama hizi nyekundu na njano. Tuendelee kuelimisha jamii kuhusu suala la lishe, tupeleke fedha kwa wakati ili kuhakikisha suala hili linafanikiwa.” Mhe. Machali
Aidha Mkuu wa wilaya amewakumbusha wazazi wilayani Mkalama kuendelea kuwaelimisha watoto wao kuhusu suala la mimba za utotoni. “Kaeni na vijana wenu wafundisheni kuhusu mimba za utotoni na madhara yake” DC Machali
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi.Asia Messos amewakumbuha watumishi wa kada ya afya kueendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa wajawazito Kwenda kliniki mapema ili kuepukana na madhara yanayoweza jitokeza wakati wa kujifungua
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.