Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Ndugu Mohamed Atiki amewataka washiriki wa mafunzo ya Stadi za Maisha yanayotolewa na Shirika la Camfed Tanzania kuzingatia mafunzo hayo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kwa maisha yao ya baadae.
Wito huo ameutoa leo mapema wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 2 kuanzia Mei 21-22,2024 yanayofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Mkalama na kuhudhuriwa na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule pamoja na Walimu Walezi.
“Wito wangu kwa washiriki wote, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Walimu Walezi kuhakikisha mradi huu unafanikiwa ili wapate ujuzi utakaowasaidia katika Maisha yao ya baadae,kwa kushirikiana na CAMFED tunaweza kuchochea maendeleo ya jamii zetu” Ndugu Mohamed Atiki
Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Mkalama, Mwl. Said Kalima amewasisitizia walimu hao kufanyia kazi mafunzo hayo yanayotolewa na CAMFED ili kuweza kuondoa tatizo la watoto wanaoacha shule.
“Ndugu zangu walimu, sisi ndio wadau wenye mradi huu, tuhakikishe tunashirikiana pamoja ili tumkomboe mtoto wa Mkalama katika suala la kushindwa kumaliza masomo yake” Afisa Elimu Sekondari,Mwl. Said Kalima
Awali akitambulisha mradi huo,Kiongozi wa mradi wa Stadi za Maisha kutoka CAMFED, Bwana Leonard Msigwa amewaomba washiriki wa mafunzo hayo kuupokea mradi huo kwa mikono miwili kwani umekuwa na mafanikio makubwa katika kuboresha maendeleo ya wanafunzi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.