Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos amewataka wananchi wilayani Mkalama kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2024.
Wito huo ameutoa Agosti 26,2024 wakati wa ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa vijiji vya Gumanga na Nduguti wilayani hapa
“Nawasihi msipoteze haki zenu za msingi, utakapofika wakati wa kujiandikisha, mjiandikishe, utakapofika wakati wa kampeni jitokeze na itakapofika wakati wa kupiga kura Novemba 27, 2024 tujitokeze kuwachagua viongozi wetu tunaowataka” Bi. Asia Messos
Akizungumzia suala la maadili, Bi.Asia Messos amewakumbusha wakazi wa vijiji vya Nduguti na Gumanga kuwa mstari wa mbele kupinga mila na desturi zinachochea mmomonyoko wa maadili katika jamii.
“Tujikite sana katika malezi yetu, turudi katika misingi yetu ya kitanzania. Hii iwe ajenda kubwa katika mikutano yetu, katika nyumba zetu za ibaada. Tuungane pamoja kupinga ushoga na usagaji katika jamii zetu” Bi. Asia Messos
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mkalama amewataka wazazi wilayani hapa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule kwa manufaa ya maisha ya baadae pamoja na kusisitiza suala la kuchangia chakula shuleni.
Awali akielezea mambo makubwa yaliyofanywa na serikali katika miaka 3 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bi. Asia Messos amesema Halmashuri ya wilaya ya Mkalama imepokea zaidi ya bilioni 60 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ya elimu,afya umeme,Barabara pamoja na kilimo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.