Katibu Tawala wilaya ya Mkalama Ndugu Peter Masindi amewataka watumishi wa Afya mkoani Singida kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuweka mikikati endelevu itakayo saidia kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.
Kauli hiyo ameitoa Oktoba 30, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama katika kikao kazi cha siku 2, kuanzia Oktoba 30-31, 20204 cha kujadili vifo vya Mama na Mtoto mchanaga kwa mkoa wa Singida kwa robo ya kwanza Julai 1-Septemba 30 kilichofanyika katika ukumbishi wa Sheketela wilayani Mkalama.
“Twendeni tufanye kazi kwa bidii ili kuondoa tatizo hili katika mkoa wetu, tutumie vizuri kikao hiki kukabiliana na vifo vya kina mama na watoto wachanga katika mkoa wetu wa Singida” DAS Masindi.
Aidha Ndugu Masindi amewakumbusha watumishi wa afya kuwa na lugha nzuri kwa kina mama wanaofika katika vituo vya kutolea huduma za afya kupata huduma mbalimbali “Tusisahau kuwa na lugha nzuri kwa wateja wetu, kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetimiza lengo la serikali la kuboresha huduma kwa wananchi” Ndugu Masindi
Kwa upande wake Mratibu wa afya Uzazi na Mtoto Mkoa Wa Singida, Christoweru Barnabas amesema kupitia kikao hiki watapata ufumbuzi wa namna wa kupunguza hali hii pamoja na kuwataka kina mama mkoani Singida kuanza mapema kliniki ili kuepusha madhara vifo hivi vya Mama na Mtoto Mchanga.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.