• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAKABIDHI KADI ZA MATIBABU BURE KWA WAZEE MKALAMA

Imewekwa kwenye: June 15th, 2025

Jumla ya wazee 20 kutoka Wilaya ya Mkalama wamekabidhiwa kadi za msamaha wa matibabu bure wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili kwa Wazee Duniani kwa Mkoa wa Singida, yaliyofanyika Juni 15,2025 katika ukumbi wa Sheketela uliopo  Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali, aliwataka wazee kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kusimamia maadili na malezi bora ya watoto, pamoja na kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

“Tunayoyaona leo ni matokeo ya malezi yetu. Tulishindwa kuwasimamia watoto wetu vizuri, matokeo yake tunaona baadhi ya watoto wamewatelekeza wazee wao,” alisema Mhe. Machali.“Nitumie nafasi hii kuwahimiza wazee kuwasimamia watoto wao wenye watoto katika malezi, ili tuepukane na changamoto kama hii.”Mhe. Machali aliwakumbusha wazee kutumia ofisi za Ustawi wa Jamii zilizopo katika halmashauri zao kama njia rasmi ya kuripoti vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanavyofanyiwa, badala ya kuvumilia kimya kimya hali zinazowakandamiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Singida, Mchungaji Mbura Joel, alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zinazofanyika katika kulinda haki na ustawi wa wazee nchini.

Akizungumza kuhusu kadi hizo za msamaha wa matibabu, Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Mkalama, Bi Mwajuma Yusuphu, alisema kuwa kadi 20 zilizotolewa leo ni sehemu ya jumla ya kadi 5,000 zilizotolewa kwa wazee mbalimbali wilayani humo kuanzia Julai 1, 2024 hadi Juni 2025.

Maadhimisho hayo yalilenga kuhamasisha jamii kutambua, kulinda na kutetea haki za wazee sambamba na kuhakikisha kuwa kundi hilo linaishi kwa heshima, usalama na upendo katika familia na jamii


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YAKABIDHI KADI ZA MATIBABU BURE KWA WAZEE MKALAMA

    June 15, 2025
  • SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MKALAMA

    June 16, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkalama Apongeza Ujenzi wa Zahanati ya Nkenke

    June 13, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA

    June 11, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.