Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge ameipongeza menejimenti ya halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa namna walivyojibu hoja za mkaguzi Mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali jambo alilotaja kuwa ni ushirikiano Mkubwa kwaajili ya masilahi ya wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Rc. Mahenge alisema hayo mapema leo katika kikao cha Baraza la madiwani la hoja lilifanyika katika ukumbi wa sheketela uliopo halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
‘’Halmashauri ya wilaya ya Mkalama sina maneno mengi kwa sababu mnafanya kazi nzuri na moja ya kipimo cha kazi nzuri iko kwenye ukusanyaji wa mapato, na mwezi wa tatu kulifanyika tathimini ya mapato kati ya halmashauri zilizofanya vizuri Mkalama nayo ilikuwepo hii inadhihirisha kuwa mnafanya kazi kwa kushirikiana na hadi sasa mna asilimia 95% ya ukusanyaji wa mapato niwapongeze sana kwa kazi nzuri mnayoifanya’’ Aliongeza Rc Mahenge.
Hata hivyo aliagiza watumishi wote wa halmashauri kuwa na taarifa ya fedha zote zilizotumika kwenye miradi na kuzisambaza kwa madiwani ili wajue fedha zilizotumika katika kata zao na kurahisisha ufuatiliaji kwa kila hatua.
Pamoja na hayo aliendelea kupinga vikali suala la Wanganga wa jadi wanaotumia ramli chonganishi ( LAMBALAMBA) wilayani hapa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na sheria za Nchi kwani wanapita kwa wananchi na kuwachangisha fedha ili kuwatibu suala hilo halikubaliwi kwani linavunja amani na kuchochea chuki kwa wananchi.
Hata hivyo aliwaagiza madiwani kusimamia suala hilo kwenye Kata zao huku akitoa onyo kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo alitumia fursa hiyo kuwataka madiwani pamoja na viongozi mbalimbali wilayani Mkalama kuwasisitiza wananchi kutunza akiba ya chakula walichonacho ili wilaya isije ikakubwa na njaa kutoka na mvua kunyesha chini ya wastani hivyo kupelekea baadhi ya maeneo kuwa na uhaba wa chakula.
Awali akisoma taarifa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos alisema kati yahoja 51 zilizoibuliwa na Mkaguzi mkuu wa serikali tayari 27 zimejibiwa kikamilifu huku zingine 24 zikiwa hazijabiwa kikamilifu na kuongeza kuwa Menejimenti ya wilaya ya Mkalama imejipanga kikamilifu kujibu hoja hizo huku wakihakikisha wanaziba mianya ya kuibuliwa kwa hoja mpya.
Diwani wa kata ya Mwangeza Bosco Samwel ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama alisema kuwa uongozi wa wilaya ya Mkalama kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali wilayani hapa watahakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuendelea kupata hati safi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.