MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, amewagiza Wakuu wa Wilaya wapya waliotambulishwa mkoani hapa kwenda kutatua matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao ikiwamo migogoro ya ardhi pamoja na kuhakikisha wanaongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Ametoa agizo hilo leo (Februari 7, 2023) wakati akiwatambulisha wakuu wa wilaya wanne waliohamishiwa mkoani hapa ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson, Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Joshua Nassari, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali na Mkuu wa Wilaya Manyoni, Kemilembe Lwota.
Aidha amesema mkoa una migogoro mingi ya ardhi hivyo namna pekee ya kutatua changamoto hiyo ni kuimarisha ushirikiano baina ya viongozi na wananchi na kudhibiti vitendo vya rushwa ili kuwapatia haki kwa kila anaye stahili.
Pamoja na hayo Serukamba amewataka wakuu hao wa wilaya kusimamia suala la mapato kwa kuwa bado inaonekana uwepo wa mianya ya ubadhirifu wa fedha za serikali, ambapo ameelekeza kufanya uchunguzi kwenye minada na leseni za biashara kwani huko ndiko kwenye upotevu mkubwa wa fedha.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.