Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 16 amezindua mradi wa Daraja la Msingi , Kijiji cha Kidii Kata ya Msingi Wilaya ya Mkalama lenye thamani ya Tsh. Bill 11.1 ambapo ametaja litachochea maendeleo ya Wilaya.
Baada ya kuzindua daraja hilo Rais aliongea na Wananchi wa Wilaya ya Mkalama ambapo aliwataka kutumia daraja hilo kuchochea uchumi wa Wilaya kwakuongeza uzalishaji katika Kilimo pamoja na biashara kwani kuna uhakika wa usafiri na usafirishaji unaounganisha Mikoa ya Singida, Simiyu , Tabora na Mara .
Pamoja na hayo Mhe. Dkt. Suluhu ameipongeza Wilaya ya Mkalama kukua kwa kasi kimaendeleo pamoja na kuwa Wilaya changa ya Mkoa wa Singida ambapo aliwataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidi ili kuchochea zaidi maendeleo hayo.
‘’Wilaya ya Mkalama ni Wilaya changa , lakini pamoja na uchanga wenu Wilaya inakua kwa kasi na mnalingana kimaendeleo na Wilaya kongwe’’ Alisema Dkt. Samia
Pamoja na hayo Mhe. Dkt . Samia amesema Serikali kuu imejidhatiti kwa dhati kuwekeza katika Sekta mbalimbali ikiwepo Afya, Elimu, Kilimo, Mifugo na uvivu , ambapo amesema inaendelea kutatua changamoto huku akiahidi Neema ya ujenzi wa nyumba za walimu kwenye bajeti ya 2024/2025 .
Sanjari na hayo Mhe. Dkt . Samia aliwataka wananchi kuendelea kulinda Amani iliyopo kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 ambapo amewataka kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo.
Ziara ya Mhe, Rais ni mwendelezo wa Ziara yake Mkoani hapa ambapo ametembelea na kuzindua Miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani hapa na atahitimisha kesho Oktoba 17 2023 katika Wilaya ya Iramba.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.