Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amewataka wakusanya mapato kuwa waadilifu katika kazi yao ili kuongeza pato la Wilaya na sio kutumia nafasi hiyo kujinufaisha.
Amesema hayo mapema leo November 11 2022 katika hafla ya kukabidhi mashine 20 za Kielektroniki za kukusanya mapato (POS) kwa wakusanya mapato katika ukumbi wa Mkuu wa wilaya ya Mkalama.
‘’mkakusanye ushuru ili kuongeza pato la Halmashauri, naomba msitumie nafasi hii kujinufaisha. Mkiamua kufanya kazi kila mmoja atafanya kazi yake kwa weledi bila kusukumwa wala kutishwa maana aliye waajiri ninyi ni Halmashauri na wala sio mtu mwingine’’. Aliongeza Dc Kizigo.
Aidha aliwataka wakusanya mapato hao kuweka fedha Benki ndani ya masaa Ishirini na Nne (24) ili kuepuka ubadhilifu wa fedha utakaojitokeza dhidi yao.
‘’Tunawategemea katika kukusanya mapato, mwaka huu tunategemea kukusanya kiasi cha Billioni moja na Millioni Mia tano, hadi kufikia Oktoba 30 tayari tulishakusanya asilimia Thelathini na Saba (37%) tumekubaliana na Waheshimiwa Madiwani hadi kufikia tar 30 Disemba tutakuwa tumekusanya Zaidi ya 50% na wakusanyaji ndio nyie na ili kufikia hizo Asilimia hakikisheni ndani ya masaa Ishirini na nne mnaweka fedha benki ili kuepuka ushawishi wakutumia kwenye matumizi yasiyo rasmi.’’ Alisema Dc Kizigo.
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya Afisa Mapato wa Wilaya ya Mkalama Jean Claude Gowelle alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama imekuwa ikikusanya mapato yake kwakutumia mashine za POS kwa kila chanzo cha mapato katika vizuizi vya ukaguzi wa mazao, ukaguzi wa Nyama pamoja na Minada.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.