Maafisa Elimu Kata, Wenyeviti wa Bodi za Shule, Wakuu wa Shule za Sekondari pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi wamepatiwa mafunzo ya uongozi leo tarehe 16/02/2026 yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sheketela, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Elimu Msingi wa Wilaya ya Mkalama, Bi. Jusline Bandiko, amewahimiza washiriki kutumia ipasavyo maarifa waliyoyapata katika kuimarisha usimamizi wa shule, kuongeza uwajibikaji na kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama za kuimarisha sekta ya elimu na kuhakikisha utoaji wa huduma bora za elimu kwa wanafunzi wote.
#ElimuKwanza
#UongoziBora
#MkalamaKazini
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.