ONGEZENI UZALISHAJI WILAYANI MKALAMA ' RC SERUKAMBA '
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba amewataka Wananchi wa Kijiji Cha Hilamoto , Dominiki , Munguli , Mwangeza na Ikolo Kata ya Mwangeza Wilaya ya Mkalama kuongeza maeneo ya Kilimo katika kipindi cha Kilimo Ili kuongezea uzalishaji Wilayani hapa na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja, Wilaya na Mkoa kwa ujumla.
Amesema hayo mapema Leo Novemba 09, 2023 katika ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo , kusikiliza na kutatua kero za Wananchi aliyoifanya leo Wilayani hapa.
Aidha Mhe. Serukamba amesema lengo la serikali ni kuhakikisha Wananchi wanakuwa na uchumi mzuri pamoja na huduma muhimu Kwa kusogeza huduma karibu ikiwepo pembejeo za Kilimo ambapo aliwasisitiza Wananchi kuendelea kujisajili katika daftari Ili waweze kununua mbolea ya ruzuku kwa bei ya punguzo.
Amesema kuwa lengo la kuongezea uzalishaji kwa wakulima ni kupambana na hali ya umasikini Mkoani hapa na kuwaeleza endapo Kila Mkulima ataongeza maeneo ya kulima watapelekea kukua kwa Uchumi pamoja na kuboresha maisha yao.
"Niwasihi Wananchi ongezeni maeneo ya kulima, tulime alizeti kwa wingi, Kitunguu , Mahindi, dengu na mazao mengine Ili Mkoa wetu uwe katika hali zuri ya uchumi " Alisisitiza Serukamba .
Pia amewataka kulima Kilimo cha kisasa na chenye tija kwakutumia mbolea pamoja na mbegu bora ili kuongezea uzalishaji.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutatua kero mbalimbali za Wananchi ndio maana anapita kijiji kwa kijiji kuhakikisha kero za Wananchi zinatatuliwa kama sio kumalizwa kabisa.
"Serikali inatatua kero za wananchi ndio maana Leo mnaniona nipo hapa " Alisisitiza Serukamba Rc Singida.
Pamoja na hayo ametumia mikutano hiyo kuwataka Wananchi kuacha kuuza mazao yakiwa Shambani na kuwataka kujiunga kwenye vyama vya ushirika Ili kuwa na bei elekezi itakayowafanya madalali kukosa soko kwani wamekuwa wakiwatumia wakulima hao kujinufaisha wenyewe.
Sanajari na hayo amewataka Wananchi Wilayani Mkalama kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa mlipuko wa homa ya kutapika na kuharisha ( Kipindupindu) kwa kuzingatia usafi wao binafsi na mazingira yao wanakoishi kwakuwa na vyoo bora.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.