Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi.Asia Messos akiwa na Wakuu wa Idara, Vitengo na Taasisi za Umma, leo Septemba 6,2024 ameefanya ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Kata za Msingi na Kinyangiri wilayani hapa
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kinyangiri na Msingi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama amewataka wananchi wa kata hizo kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27,2024.
"Mwaka huu tuna tukio kubwa muhimu kwa ajili ya maendeleo yetu, ni uchaguzi wa Serikali Za Mitaa. Nitumie nafasi hii kuwasihi kushiriki kwa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi pamoja kupiga kura kuwa chagua viongozi tunaowataka, ifikapo Novemba 27,2024 kwa pamoja twende tukapige kura" Bi.Asia Messos
Akizungumzia kuhusu zoezi la uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Bi. Asia Messos amesema kuwa zoezi hilo litaanza Septemba 25,2024 kwa mkoa wa Singida na litachukua muda wa wiki moja kwa wananchi kuboresha taarifa zao pamoja na kujiandikisha kwa wale waliofikisha umri wa miaka 18, "Kipekee naomba mjitokeze kwa wingi kuboresha taarifa zenu kwa ajili ya uchaguzi wa 2025 wa Rais,Wabunge pamoja na Madiwani"DED Asia
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Bi. Asia Messos, amewakumbusha wakazi wa kata hizo juu ya muhimu wa kulinda maadili, kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, wajawazito kufika kliniki kwa wakati pamoja na kulinda miundimbinu ya miradi inayojengwa na serikali.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.