Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amewaagiza Maafisa Ugani, watendaji wa Vijiji na Kata wa Wilaya ya Mkalama kuhakikisha ndani ya wiki mbili wanakusanya fedha za Mbegu za Alizeti walizokopeshwa wakulima wa Mkalama kwa msimu wa kilimo mwaka 2022/23 zinakusanywa mara moja na kupeleka fedha hizo Benki na wakuwasilisha stakabadhi ya Malipo ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Agizo hilo amelitoa Disemba 1/2023 katika mkutano na wakuu Idara, Maafisa Ugani, Watendaji wa Vijiji Na Kata uliofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
‘’niwaambie tu hizo pesa mlizokusanya kwa wakulima hazitakuwa na msamaha tena kama ilivyokuwa kwenye msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022, kwani serikali iliona mbegu za ruzuku iliyotoa haikufanya vizuri’’ Alisisitiza Dc Machali.
Amesema kwa mujibu wa maafisa Kilimo Wilaya inahitaji tan 1500 za mbolea na hadi sasa ni Tani 1400 zimefika kwahiyo bado kuna mapungufu kidogo ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwapongeza Maafisa hao kuhamasisha wakulima kuanza kutumia mbolea ili kuongeza uzalishashi Wilayani hapa.
Mhe. Machali amewasisitiza Wakulima kila mmoja kuhakisha anakuwa na kitambulisho cha Taifa au namba za Nida ili kuepusha usumbufu unaojitokeza kwenye mfumo kwa baadhi ya Wakulima kuwa na namba moja ya Nida zinazofanana na kupelekea wengine kukosa ruzuku ya mbolea
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.