MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA SH. BILL. 1.7
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalah Shaibu Kaim amewataka wananchi kuitunza miundo mbinu yote iliyozinduliwa leo September 23, 2023 na mwenge wa uhuru kwa maendeleo na ustawi wa kizazi kijacho.
Ameyasema hayo mapema leo wakati akiongea na wananchi wa Wilaya ya Mkalama baada ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo .
Mwenge umezindua miradi ya ujenzi wa shule mpya ya Nkindiko uliogharimu shilingi Mil. 493.4 wenye madarasa 16 pamoja na Jengo la utawala na matundu 20 ya vyoo, umeweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kijiji cha Malaja kata ya Nkalakala wenye Thamani ya Tsh. Mil.565 ambapo ukikamilija utawanufaisha wananchi wapatao 6,611,mradi wa matengenezo ya barabara ya Mwando-Mng’anda-Mwanga Km 12.39 na Ishenga Iambi uliogharimu Mil.314.9,uzinduzi wa jengo la wagonjwa wa dharura (EMD) katika hospitali ya wilaya uliogharimu Mil.300.
Sambamba na hayo Mwenge umetembelea mradi wa Vijana wa Kilimo cha Nyanya Kikundi cha Msingi Land wenye Thamani ya Tsh. Mil 9, Kuzindua Mradi wa ujenzi wa Darasa Moja katika Shule ya Msingi Maelu Kijiji cha Kisuluiga Kata ya Gumanga ,wenye Thamani wa Tsh. Mil. 24.5, Kutembelea na kukagua program ya mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI,mapambano dhidi ya malaria,mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, lishe na mapambano dhidi ya rushwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mh.Moses Machali alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Wilayani Mkalama hivyo kuwataka wananchi kuunga Mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita kwa kuilinda miradi iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2023.
Kauli mbiu ya Mbio ya Mwenge wa Uhuru 2023 ‘Tunza mazingira,okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa’
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.