Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa madarasa Saba katika shule ya Sekondari Gumanga yaliyotekelezwa kwa fedha za Uviko 19 uzinduzi wa daraja la mawe katika kijiji Cha Minganga Kata ya Miganga , mradi wa Maji Milade Kata ya Tumuli, Uwekaji jiwe la Msingi katika kituo Cha Afya Gumanga ambayo imegharimu jumla ya TSH.Bilioni 1.34.
Pamoja na kuweka Mawe ya Msingi na kukagua miradi, Mwenge umetembelea na Kuzindua kilabu ya kupinga rushwa katika shule ya Sekondari Nduguti pamoja na kutembelea program ya lishe shule ya Sekondari Gumanga, Mapambano dhidi ya Maralia na VVU na UKIMWI na kukagua kikundi cha Vijana cha Iguguno .
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Bw. Sahili Nyanzabara Geraruma ameupongeza uongozi wa wilaya ya Mkalama Katika kutekeleza miradi ya Maendeleo vizuri huku akiwataka kufanyia kazi mapungufu yaliyobainika kwenye baadhi ya miradi.
Akiongea katika uzinduzi wa daraja la Mawe kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Geraruma amewataka wahandisi kuendeleza teknolojia ya mawe na wengine waige kwani amesema kuwa linatumia kiasi kidogo Cha fedha ikilinganishwa na mengine yanayojengwa kwa zege na nondo.
Aidha amewataka wananchi kuitunza miundo mbinu ya miradi yote iliyozinduliwa Leo Kwa Maendeleo yao pamoja na kulitunza daraja kuondoa uchafu na kulinda vyuma visiibiwe Ili kuondoa changamoto ya upitikaji wakati wa mvua Kama ilivyokuwa mwanzoni.
Hata hivyo amewataka wahandisi wa tarura ambao ndio wasimamizi wa Ujenzi wa daraja hilo kuweka viakisi mwanga ili kuzuia ajali ambazo zinaweza Kutokea wakati wa usiku.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo alieleza umuhimu wa miradi yote kuwa itatatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwepo kutatua kero ya Upatikanaji Maji safi salama katika kijiji cha Milade pamoja na changamoto waliyokua wakipata wananchi wa kata ya Miganga waliokuwa hawezi kwenda Hospitali ya Wilaya kwa Sababu ya kukatika Kwa mawasiliano ya barabara na kusema kukamilika Kwa daraja hilo litawasaidia watu wa Nkinto, Miganga na Nduguti Katika Shughuli zao za kibiashara na kijamii.
Kwa upande wake Mhandisi wa TARURA wilaya ya Mkalama Mang'ara Magoti Matiku amesema Ujenzi wa daraja hilo imegharimu Tsh. Milioni 180.5 na kuokoa TSH.milioni 639.4 kwa kuwa Kama lingejengwa kwa zege na nondo lingegharimu TSH.milioni 820.
Mhandisi Magoti amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali kupitia fedha za mfuko wa jimbo kwa mwaka 2021/22 na unatekelezwa na Mkandarasi Chase Investment wa mwanza na kazi zilizopangwa ni kuchimba kupanga mawe kushuka Chini kumwaga zege na kujenga mawe.
Pamoja na hayo Kiongozi wa mbio za mwenge Sahili Nyanzabara Geraruma aliwasisitiza Wananchi kushiriki katika sensa ya watu na Makazi kujitokeza kuhesabiwa tarehe 23 .8.2022, pia kukomesha na kutokomeza Maralia Kwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga, kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya , Mapambano ya rushwa pamoja na wanachi kuzingatia masuala ya Lishe Ili wawe na afya njema.
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Mkalama Leo ambapo umekimbizwa kilometa 129 na umekagua miradi mitano na programu tano.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.