Wilaya ya Mkalama Leo imekabidhi Mwenge wa uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida .
Akikabidhi Mwenge wa huru, Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amesema kuwa Mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Mkalama umetembelea na kukagua Miradi mitano na program tano yenye thamani ya sh Bill 1.34.
Pamoja na hayo Dc Kizigo alisema kuwa Mwenge ukiwa wilayani Mkalama umeacha jumbe mbalimbali ikiwa ni pamoja na Sensa ni Msingi wa mipango ya Maendeleo shiriki kuhesabiwa tuyafikie malengo ya taifa, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kuzingatia lishe bora, Mapambano dhidi ya rushwa ,Mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI, Mapambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.
Akiongea wakati wa kukabidhi Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bw.Emmanuel Ndege Chacha Mkimbiza Mwenge kitaifa, alisema kuwa Mwenge wa uhuru umependezwa na umoja na mshikamano wa viongozi na Wananchi wa wilaya ya Mkalama na kuwataka kuendeleza umoja huo hata baada ya Mwenge kuondoka wilayani hapa.
Aidha Bw. Chacha aliwataka Wananchi wa wilaya ya Singida kuiga mfano Kwa Mkalama kwani nyaraka zote zilizokua zinahitajika zilikua halisi na zimenyoka tena zilikua zipo kwenye maeneo ya miradi na miradi yote iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru iliendana na thamani iliyokusudiwa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Singida Mhandisi Pascasi Mragiri amekiri kupokea Mwenge wa uhuru ukiwa unawaka na kumeremeta hivyo kusema kuwa Mwenge ukiwa wilayani Singida utakimbizwa kwa Kilomita 130 na utazindua na kukagua Miradi ya Maendeleo pamoja na kutembelea program tano zenye thamani ya shilingi Bill.1.36.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.