MAAFISA ELIMU TAALUMA, TSC, WADHIBITI UBORA ELIMU NA WARATIBU ELIMU KATA , WANOLEWA NA SHULE BORA.
Katika kuboresha elimu wilayani Mkalama Mradi wa shule bora umetoa mafunzo endelevu kwa walimu kazini (MEWAKA) kwa Maafisa Elimu taaluma, Wadhibiti Ubora elimu, TSC , pamoja na Waratibu elimu kata ili kubadili mitazamo ya walimu na kupelekea matokeo chanya.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku moja katika Shule ya Msingi Nduguti iliyopo Kata ya Nduguti Wilayani Mkalama.
Mwezeshaji wa Mfunzo hayo Jasie Sijjo alisema kuwa lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo Viongozi hao na kuwa chachu kwa walimu jambo ambalo litawasaidia kujua namna ya ufundishaji na kuwasaidia walimu kuwa na elimu shirikishi kwa na jumuishi kwa kuzingatia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
‘’Miongoni mwa Malengo ya program ya Shule bora ni kuimarisha mifumo na leo tumeanza na nyie viongozi tukiamini mtapeleka chachu kwa walimu ambayo itapelekea kubadili mitazamo yao na kuleta matokeo chanya’’ Alisema Sijjo.
Aidha Bw. Sijjo aliongeza kuwa mradi wa Shule bora unatekelezwa kwa Mikoa tisa Nchini ambayo imegundulika kuwa na changamoto katika sekta ya Elimu na unatarajia kuwafikia wanafunzi takrabani Milioni Nne.
‘’mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka Saba na utawafikia wanafunzi takribani Millioni Nne , Walimu Elfu Hamsini na Nne , Shule Elfu tano Mia saba hamsini na Saba pia mabadiliko na ubunifu yataonekana na kutathiminiwa katika ngazi za chini ambazo walengwa muhimu watapatikana katika Shule zote za Msingi Nchini’’. Aliongeza Bw. Sijjo.
Naye Bi. Telise Msongole mwezeshaji katika Program ya Shule Bora aliwaelekeza Viongozi namna ya kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kama njia ya kujisomea na kupata habari mtandaoni na nakuongeza kuwa MEWAKA inaenda kufanikiwa kutokana na Viongozi hao kuwa waadilifu katika kipindi chote cha mafunzo .
‘’ kiongozi ni kuonyesha njia naamini usikivu huu na uamanifu mliounyesha Mewaka inaenda kuleta matokeo chanya kwa walimu wetu kwani viongozi mmepokea na mtaaenda kuwarithisha walimu na kupelekea matokeo chanya kwa wilaya yetu ya Mkalama na Mkoa kwa ujumla.Aliongeza Bi.Msongole.
Akiongea kwa niaba ya washiriki wote Mratibu elimu Kata ya Kinampundu Abubakari Misanga aliishukuru serikali kupitia program ya Shule bora kwa mafunzo hayo kwani yamewajengea uwezo nao watakuwa chachu kwa walimu wote ili kuhakisha kiwango cha elimu kinakuwa katika Mkoa wa Singida hivyo kuleta matokeo Chanya ka maslahi mapana ya wilaya na Mkoa wa Singida.
Program ya Shule Bora inatekelezwa kwa Mikoa ya Kigoma, Katavi, Simiyu, Singida, Rukwa, Mara, Dodoma,Tanga pamoja na Pwani na unafadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid na gharama za mradi zitakuwa na bajeti ya Paundi za Kiingereza 89 Millioni, sawa na Shillingi Billioni 270 za Kitanzania na utafanya katika ngazi zote za mradi ,Mradi huu unatekelezwa hadi ifikapo mwaka 2027.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.