Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali, leo Desemba 1, 2025 amekutana na kuzungumza na Mama Lishe pamoja na Maafisa Usafirishaji (maarufu kama Bodaboda) wa wilayani hapa katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ulipo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mkalama.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Machali amewataka Mama Lishe na Maafisa Usafirishaji kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani ya nchi kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Tanganyika, yanayofanyika Desemba 9 2025.
“Amani ikipotea gharama ya kuirejesha ni kubwa sana. Tujiepushe na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha machafuko,” amesema Mhe. Machali
Aidha Mhe. Machali amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa mapema pale wanaposikia watu wakipanga vurugu au kuhamasisha uvunjifu wa amani.
Vilevile Mhe. Machali amesema kuwa serikali serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote au kundi lolote litakalojaribu kuleta vurugu katika wilaya ya Mkalama na amesisitiza kuwa matatizo hayatatuliwi kuanzisha tatizo jingine, bali kupitia mazungumzo, umoja na kuheshimu sheria
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.