Wananchi wa vijiji vya Igonia na Kinakamba wilaya ya Mkalama wameishukuru serikali kwa kuwasogezea huduma za afya karibu kitu ambacho kitawasadia kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo
Shukrani hizo wamezitoa Agosti 10,2024 wakati wa uzinduzi wa Zahanati mpya ya Kijiji cha Kinakamba katika kata ya Ibaga pamoja na Zanahiti ya Kijiji cha Igonia inayopatikana katika kata ya Ibaga wilayani Mkalama.
Elipendo Samweli, mkazi wa Kijiji cha Igonia amesema kwa muda Mrefu wamekuwa wakitembea umbali Mrefu kufuata huduma hizo katika vijiji vya Mkalama, Gumanga na Nduguti
“Tunaishuruku sana serikali, hatukuwahi kuwa na Zahanati katika Kijiji chetu leo hii mimi kama Mama, zahanati hii itasaidia kupata huduma mbalimbali kama vile watoto kupata chanjo kwa wakati, wajawazito kufika kliniki kwa wakati, tunasema asente”
Rajabu Issa Mkumbo, makazi wa Kijiji cha Kinakamba amesema kufunguliwa kwa Zahanati hiyo itawasadia kuondoa gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo katika vijiji vya Mkalama, Nduguti pamoja na Gumanga.
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa zahanati hizo mbili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mhe. James Mkwega amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano kwa watoa huduma wanaoletwa na serikali pamoja na kuwaomba kuchangia damu kwa wingi.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa wilaya ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael amewakumbusha watumishi wa afya kutoa huduma bora na kuwasisitizia wananchi kujiunga na bima ya afya ya CHF kwa yenye gharama nafuu.
Kuzinduliwa kwa Zahanati ya Igonia pamoja na Kinakamba, kunapeleka wilaya ya Mkalama kuwa na jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya 41.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.