Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Singida Mhe.Aysharose Mattembe amegawa kilogramu Mia tano hamsini za mbegu ya Alizeti (Kg550) aina ya Record (Standard) kwa Wanawake wa wilaya ya Mkalama ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la Alizeti Mkoani Singida.
Zoezi hilo lilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Ofisi za Chama cha mapinduzi (CCM) Kijiji cha Nduguti kata ya Nduguti wilayani Mkalama katika ziara yake ya Kikazi ya kutembelea Wanawake wa Mkoa wa Singida .
Aidha Mhe.Matembe alisema kuwa serikali imekua ikitumia Fedha nyingi kuagiza mafuta ya kula nje ya Nchi ndio maana ikaja na mkakati wa kuongeza tija katika uzalishaji wa zao hilo kwa Mikoa ya Dodoma, Simiyu na Singida ya kuhakikisha zao la alizeti linalimwa kwa wingi ili mafuta yapatikane kwa wingi Nchini.
Pia amewataka wanawake kufanya kazi kwa bidii na kuongeza uzalishaji kwa maslahi mapana ya familia, wilaya na Taifa kwa ujumla.
“Naipongeza serikali yetu kuona ipo tija ya kuongeza uzalishaji wa zao la Alizeti nimeona nami niiunge mkono serikali yangu sikivu kwa kugawa mbegu hizi kwa wanawake hawa ninajua wanawake ndio wazalishaji wakuu hivyo ninawaombea mbegu hizi zikamee na kazaa vizuri ili kuongeza pato lenu wanawake na familia zenu kwaujumla’’. Aliongeza Mhe.Mattembe.
Awali akitoa elimu ya kilimo cha zao la hilo , Afisa kilimo wilaya ya Mkalama Bw.Daniel Jacobo alisisitiza kanuni bora za kilimo cha alizeti , ambazo ni kupanda kwa wakati, kutumia mbolea za Asili na za Viwandani kupalilia kwa wakati huku wakiwataka kuwatumia wataalamu pindi wanapoona mimea yao haipo kwenye hali ya kawaida.
Akitoa neno la shukurani kwaniaba ya wanawake hao Diwani wa viti maalumu wilaya ya Mkalama Mhe.Mariam Kahola alimshukuru Mhe.Mbunge kwa kuwatembelea wanawake wa wilaya ya Mkalama na kuwapatia mbegu za alizeti ili kuongeza uzalishaji wilayani Mkalama ambapo aliongeza kuwa watatumia elimu ya kilimo vizuri kwa kulima zao la alizeti na kuzingatia kanuni bora za kilimo katika kukuza pato la wilaya na taifa kwa ujumla.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.