Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amepiga marufuku kwa wafanyabiashara pamoja na wakulima wilayani Mkalama kuuza na kununua zao la Dengu nje ya mfumo wa Stakabadhi Ghalani.
Marufuku hiyo ameitoa Agosti 13,2024 wakati wa mnada wa kwanza wa Dengu uliofanyika katika ghala la mazao lililopo Nduguti kwa njia ya mfumo wa TMX ambao umeshuhudia bei kwa kilo ikiuzwa kwa shilingi 2003.282
“Lengo la serikali ni kumnyanyua Mkulima, tunaka Mkulima auze Dengu yake hapa, hivyo kuanzia leo napiga marufuku kwa mtu yeyote kununua na kuuza Dengu shambani, atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu” Mhe. Machali
Mhe. Moses Machali pia amepiga marufuku kwa wafanyabiashara kusafirisha zao la Dengu nyakati za usiku bila ya kibali kinachoonesha Dengu hiyo imenunuliwa katika Ghala “kuanzia leo marufuku kusafirisha Dengu wakati wa usiku Kwenda wilaya nyingine ikiwa hauna kibali maalumu, natoa siku saba kwa wafanyabiashara ambao walikuwa tayari wamenunua Dengu walete hapa Ghalani.” Mhe. Machali
Aidha Mhe. Moses Machali amewataka wakulima wilayani Mkalama kuzingatia kanuni za kilimo bora kwa kutumia mbolea kwa wingi ili waweze kupata mazao mengi na kupelekea kukuza Uchumi wao.“Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kunyanyua sekta ya kilimo nchini, nawasihi wakulima nendeni mkajindikishe, serikali ipo kwa ajili yako Mkulima, tumieni fursa hii vizuri” Mhe. Machali
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.