• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Mafunzo ya chanjo kwa Kamati ya Afya wilayani Mkalama yaanza kuzaa matunda

Imewekwa kwenye: September 29th, 2021

L

MAFUNZO yaliyotolewa kwa Watoa Huduma wa Afya wa wilaya Mkalama mkoani Singida kwa ajili ya kutoa elimu  dhidi ya Uviko 19 kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo na kupokea chanjo yamezaa matunda baada ya baadhi ya wahudumu hao kuelewa na kuchoma chanjo hiyo hivyo kuwa mabalozi wa kwenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi.

Mafunzo hayo yalitolewa katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya wilaya ya Mkalama  kutoka kwa timu ya uhamasishaji wa chanjo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI)

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo ya chanjo kwa Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo alisema changamoto ya wananchi kutojitokeza kwa wingi kwenda kupata chanjo hiyo kwa idadi ya watu 10 inaweza kuwa ni moja ya sababu iliyosababisha wilaya hiyo na zingine hapa nchini kuwa na idadi ndogo ya watu walioitikia mwito wa kupata chanjo.

" Utaratibu wa kutoa chanjo hiyo ilikuwa wapatikane watu 10 ili dawa itakayotumika isiweze kuharibika hivyo watoa huduma walikuwa wakisubiri ifike idadi hiyo ndipo watoe chanjo,". alisema Kizigo.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) Idara ya Jamii  na Lishe, Dinah Atinda alisema uelewa na uhamasishaji mdogo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan umechangia kwa kiasi kikubwa watu kutojitokeza kwa wingi kwenda kuchanjwa.

" Serikali imetumia fedha nyingi kuagiza chanjo lakini wananchi bado hawaja kwenda kuchanjwa hivyo imetengeneza mpango mkakati harakishi wa kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu chanjo ya Uviko 19 na kuchanja" alisema Atinda.

Alisema hatua iliyofikiwa na Serikali ni kuanza kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya Taifa hadi kuwafikia walipo wananchi.

Richard Magodi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Mpango wa Taifa wa Chanjo alisema baada ya kutokea vifo vingi maeneo mbalimbali duniani kutokana na ugonjwa huo sasa hivi vifo hivyo vimeanza kupungua kutokana na kutumia chanjo.

" Na sisi kama nchi na pia Taifa ambalo lipo miongoni mwa mataifa mengine lilikuwa ni jukumu letu kuishauri Serikali na kuanzisha mpango huu wa chanjo," alisema Magodi.

Magodi alisema chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote baada ya kuhakikiwa na wataalamu na tayari imetolewa nchi mbalimbali duniani.

Wakizungumza baada ya kupata mafunzo hayo Mchungaji Setina Kanga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  (KKKT) Usharika wa Dumanga alisema sasa anakwenda kuwaeleza waumini wake umuhimu wa kupata chanjo hiyo.

Kaimu Sheikh wa Wilaya ya Mkalama Hamisi Ramadhani alisema awali alikuwa alielewi zoezi hilo la chanjo kutokana na kuwa na maneno mengi ya kukanganya lakini sasa anakwenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi.

Makamu  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama  Mhe. Bosco Samwel aliwataka washiriki wote waliopata mafunzo hayo kwenda kuhamasisha wananchi katika maeneo yao ili wapate chanjo hiyo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliopata chanjo hiyo ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ibrahim Pazia, Afisa Elimu Taaluma Sekondari, Ernest Stephen, Kalisti Faustin ambaye ni Muuguzi, Nyandewa Zabron, Afisa Muuguzi Salum Mputa, Farida  Seleman, Aizack Zabron.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YAKABIDHI KADI ZA MATIBABU BURE KWA WAZEE MKALAMA

    June 15, 2025
  • SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MKALAMA

    June 16, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkalama Apongeza Ujenzi wa Zahanati ya Nkenke

    June 13, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA

    June 11, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.