
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mohamed Hamis, amewataka Madiwani wa wilaya hiyo kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wananchi kulima kwa wingi kwa kuzingatia kilimo cha kisasa ili waweze kukuza vipato vyao.
Wito huo ameutoa Desemba 2, 2025, wakati wa Kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

“Tumefika kwenye kilimo, tuhamasishe watu walime. Wilaya yetu tuna shughuli mbili: kilimo na ufugaji. Tukihamasisha watu walime, wakilima wataondokana na umasikini,” alisema Mhe. Mohamed.
Aidha, Mhe. Hamis alisisitiza umuhimu wa wakulima kujiunga katika vyama vya ushirika ili waongeze tija na kupata faida zaidi kupitia kilimo.
“Ushirika ni jambo muhimu sana, tuhamasishe wakulima wajiunge katika vyama vya ushirika,” aliongeza.
Akizungumzia sekta ya ufugaji, Mhe. Mohamed aliwataka madiwani kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu ufugaji wa kisasa ili kuongeza tija na ubora wa mifugo yao.

OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.