Kamati ya Lishe Wilayani Mkalama wametakiwa kuandaa bajeti itakayotosheleza kutekeleza Afua za Lishe na kuingizwa kwenye Bajeti kuu 2023/2024 na katika mipango ya Halmashauri.
Akifungua mafunzo ya kamati ya Lishe wilaya jana Novemba 15. 2022 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Afisa Uchaguzi Wilaya, Bw. Abdalah Njelu alisema bajeti hiyo ifanywe kwakuzingatia vipaumbel vya Lishe ili kuondoa utapiamlo Wilayani hapa.
‘’Niwapongeze Idara ya Afya kupitia Sekta ya Lishe kufanya maandalizi ya kupata bajeti ihusuyo masuala ya Lishe hii itawasaidia kutekeleza majukumu yenu vizuri kwa wakati tofauti na hapo awali mlipokuwa manataka kufanya vikao vyenu mnashindwa kutokana na ufinyu wa bajeti’’ Aliongeza Bw. Njelu.
Pamoja na hayo aliendelea kuwataka wajumbe wa kamati hiyo kila mtu kwa nafasi yake kuhahikisha kuwa na ushindani wa kisekta katika masuala ya Lishe na kuwa kielelezo kuanzia kwenye kaya zao, pia kuhakikisha fedha zilizotengwa kwaajili ya shughuli ya Lishe zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Afisa Lishe Wilaya ya Mkalama Bi. Eliwandisha Kinyau alieleza Vipaumbele vya Halmashauri katika Lishe kwa mwaka 2022/2023 kuwa ni kupunguza Utapiamlo, kuongeza upungufu wa Virutubisho, Kuimarisha mazingira wezeshi na kutekeleza Afua wezeshi na Mtambuka.
Aidha aliendelea kwakusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama inategemea kutengeneza mpango wa bajeti utakaokidhi mahitaji ya Kibajeti na yanayozingatia afua za Lishe katika Sekta Mtambuka na kuboresha Mapungufu yaliyojitokeza katika bajeti iliyopita.
Naye Mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto Mkoa wa Singida, Bi. Christowelu Barnabas alitumia kikao hicho kuwataka Wataalamu kwa kushirikiana na sekta zingine kuendelea kutoa Elimu juu ya lishe kwa wananchi wote, ambapo Idara ya Maendeleo ya jamii kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe na ulaji unaoshauriwa kitaalamu, Idara ya Kilimo kuelimisha jamii kulima kilimo cha vyakula lishe ili jamii iwe na uelewa kuhusu lishe na kuwa na vizazi vyenye afya bora.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.