Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe.Moses Machali amewataka Watendaji wa Kata , vijiji pamoja na wasimamizi wa Lishe ngazi ya Wilaya, Kata na Jamii kuhakikisha wanasimamia vyema masuala ya Lishe kwenye maeneo yao ili kujenga jamii ya watu imara na wenye akili timamu .
Mhe. Machali, ameyasema hayo mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mkalama mapema leo November 10, 2023 katika kutathimini hali ya Lishe Wilayani hapa kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/2024 kuanzia Julai-Septemba 2023.
Amesema kuwa suala la Lishe ni ajenda muhimu inayotakiwa kuhubiriwa popote ili jamii iweze kuboresha afya zao, na kuendelea kutoa elimu ya kuchangia chakula shuleni kitakachopelekea wanafunzi kula walau mlo moja kwa siku wanapokuwa masomoni ili kuwapa utulivu wawapo darasa .
‘’Mkawaelimishe wananchi kuchangia chakula shuleni, waelezeni madhara yanayowapata watoto wakiwa na njaa, msiwachukulie hatua kama hamjatoa elimu’’. Alisistiza Mhe. Machali.
Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya utekelezaji Afua ya Lishe katika Wilaya ya Mkalama Afisa Lishe kutoka kitengo cha Lishe Idara ya afya Bw. Zacharia Nyahende amesema kuwa kitengo kinaendelea kutoa elimu ya lishe kwa makundi mbalimbali katika jamii ikiwepo kundi la wa Mama Wajawazito, Wanaonyonyesha, Watoto chini ya miaka mitano, makundi ya Wazee na Watu wazima , vijana wa rika balehe pamoja Lishe shuleni.
Ameongeza kuwa wanaendelea kuishauri jamii kula mlo kamili kwakuzingatia makundi matano ya chakula ambayo ni Nafaka , mizizi na ndizi mbichi ,asili ya wanyama na jamii ya mikunde, mbogamboga, matunda pamoja na sukari, asali na mafuta, kunywa maji ya kutosha kula mlo unaoshauri kiafya pia kufanya mazoezi.
Sanjari na hayo amesema kwa robo ya kwanza julai hadi Septemba wilaya ya mkalama imetekeleza siku ya elimu ya afya na lishe kwa asilimia 100 ambapo vijiji vyote 70 vya wilaya ya Mkalama vimetekeleza siku hiyo kupima hali za afya na lishe na kuendesha masomo ya mapishi darasani kwa jamii na jumla ya wanawake 46490 wamepata elimu.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.