Jamii imetakiwa kuwekeza kwenye elimu ili kujenga kizazi cha wasomi na kinachoweza kujitegemea , pia kuleta mageuzi ya kiuchumi , Kifikra ,kwenye jamii na taifa kwaujumla.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amesema hayo July 28 2022 katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya Awali na Msingi Nduguti (NPPEMS) yaliyofanyika mapema leo shuleni hapo katika Kijiji cha Nduguti kata ya Nduguti Wilayani Mkalama.
Aidha Mhe. Kizigo alisema kuwa elimu ni msingi wa kila kitu endapo jamii itawekeza katika elimu itatengeneza jamii yenye uwezo mkubwa wa kupambanua mambo mbalimbali na kujenga kizazi cha wasomi kitakacho kuwa msaada mkubwa kwa taifa.
Pamoja na hayo aliupongeza uongozi wa Shule ya awali na Msingi Nduguti kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la nne na kusema matokeo hayo yanatoa dira chanya kwa matokea ya darasa la saba hivyo kuwata watahiniwa hao kujiandaa kikamilifu na masomo ya Sekondari kuweza kuingia kwenye ulimwengu wa wasomi wenye ushindani mkubwa.
Dc Kizigo aliwapongeza wazazi kwakushirikiana na walimu katika kuboresha taaluma shuleni hapo huku akiwataka wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao ili kutambua watu wanao Mshirikiana na watoto , kuwa fahamu vizuri tabia zao na mienendo yao.
Awali akisoma Risala kwa mgeni Rasmi mkuu wa Shule hiyo Mwl Jackline Mushy alisema maendeleo ya taaluma shuleni hapo yamekua yakiridhisha kwani toka mwaka 2019 hadi 2021 matokeo ya darasa la Nne wamekua wakifaulisha kwa asilimia mia moja (100)
Aidha Mwl Jackline alitaja ufaulu huo mzuri unachangiwa na juhudi za wazazi , walimu , Wanafunzi pamoja na Maafisa elimu ambao wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu maendeleo ya shule hiyo ambapo aliahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa maslahi mapana ya wilaya ya Mkalama na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na mafaniko hayo Mwl Jackline alitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na ubovu wa miundo mbinu ya barabara ya kwenda shuleni , kutopewa nafasi katika ziara za kimasomo, pamoja na ushirikishwaji duni wa vikao vya taaluma vinavyofanyika wilayani hapo .
Sanjari na hayo aliwashukuru wazazi na walimu kwa ushirikiano wanaouonesha na kuunga mkono juhudi zinazotolewa na shule hiyo ambapo amesema wataendelea kutoa elimu bora kuhakikisha taaluma wilayani hapa inakua na kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya Elimu Nchini.
Shule ya awali na Msingi Nduguti ina takribani ya wanafunzi mia mbili (200) kati ya hao wanafunzi 18 ni watahiniwa wa darasa la Saba na wanatarajia kufanya mitihani yao ya kuhitimu mapema mwezi wa kumi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.